Description
Wanafunzi wa kiwango hiki huvutiwa sana na picha. Hivyo basi mwandishi amejaribu kutumia picha kadha wa kadha ili kuwasilisha kazi yake. Walimu wanfaa kufunza kwanza stadi za kusikiliza, kuongea na kusoma kabla ya kuandika. Stadi hizi nne, zinaingiliana na kujengana kwa ukaribu sana.
Ni wazi na jahara kama pengo kuwa, mwanafunzi mwenye umahiri wa kusikiliza, kuzungumza na kusoma atakuwa mahiri pia katika kuandika.